Utafiti‎ > ‎

Utafiti Unaotarajiwa

 
Utafiti juu ya mitazamo ya utawala wa serikali za mitaa
Wanajamii wanaelewa nini kuhusu wajibu/umuhimu  wa serikali za mitaa? Ni kwa kiasi gani wanawaamini watendaji wa serikali,wawakilishi wa kuchaguliwa,viongozi wa kanisa,n.k? Wanaelewa nini kuhusu haki zao? Na jinsi gani watendaji wa serikali za mitaa wanaelewa wajibu/umuhimu wao? Katika mradi huu tunafanya utambuzi/utafiti wa wanajamii na viongozi kujibu maswali yote  haya na zaidi .Hii itatusaidia kuweza kuelewa vizuri mazingira ambayo Daraja inafanya kazi,na kupanga shughuli zetu kama inavyotakiwa.