Utafiti‎ > ‎

Utafiti Uliomalizika

2006 - Kuratibu mwitikio wa jamii iliyo vijijini kwenye Virusi Vya UKIMWI / UKIMWI:  
Utafiti huu unalenga kujifunza kwa kina uzoefu wa kamati za ngazi ya kijiji za VIRUSI VYA UKIMWI/UKIMWI Tanzania.Ulifanywa na mwanzilishi wa Daraja, Ben Taylor, kwa ajili ya Daraja na kama sehemu ya mafunzo kwa utafiti ya shahada yake ya juu ya Maendeleo ya Kimataifa.
 
Utafiti unapatikana hapa kataka miundo miwili.Toleo fupi linaloeleweka ni kurasa ya kazi ambayo ilichapishwa na HakiElimu ,taasisi ya haki na Elimu Tanzania.Toleo kubwa zaidi ni Taarifa ya utafiti mzima. 
 
Fungua taarifa ya Utafiti mzima
 
 
2007-Mchanganuo wa Hali ya Mazingira ya Utawala Bora katika Serikali za Mitaa
Mapitio haya yanajengwa kwenye matokeo ya utafiti hapo juu kwa kuukuza/kutanua mtazamo ili kujumuisha sekta mbalimbali na ngazi mbalimbali za serekali. 
 
 
 
2008-Mapitio ya Upande wa Uwajibikaji kwa Jamii
Utafiti huu wa Gemma Mckenna wa chuo kikuu cha Manchester Uingereza ulileta uzoefu wa taasisi zinazotumia mfumo/njia inayofanana kwa Daraja.Mafanikio na mapungufu wa njia za miradi mbalimbali ,pamoja na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za umma ,kadi zinazoonyesha mapendekezo ya jamii, na radio ya jamii,zilichanganuliwa.Toleo fupi la taarifa ya mwisho  imechapishwa kama karatasi ya kazi ya HakiElimu.