Kazi Zetu‎ > ‎

Kutia Presha ya Maji

Mradi huu wa miaka mitatu unahamasisha wananchi kutia msukumo kwa serikali kutatua matatizo ya upatikanaji maji vijijini,teknolojia ya simu imeanzishwa ili kutengeneza njia rahisi ya wananchi kushiriki. Baada ya hapo chombo cha habari kitatumika kutoa taarifa ya mahitaji yao(kupaza sauti zao) na kuongeza uwajibikaji wa serikali kwenye huduma ya maji,katika mtizamo wa kurekebisha/kufanyia matengenezo vyanzo vya maji vilivyoharibika na kuhakikisha fungu jipya la fedha kwaajili ya upatikanaji wa huduma ya maji linatumika vizuri/ipasavyo.
 
Maboresho timilifu katika upatikanaji wa huduma hayaletwi/hayatokani na mradi wenyewe,bali na serikali,katika kuitikia msukumo/kuwajibika wa/kwa wananchi wanaoguswa na mradi.Kwa njia hii mradi unaainisha/unatatua sababu za kisiasa za uwekezaji usio na malengo na  uendelevu mbovu, na sio dalili za matatizo.Na kwa kuwaonyesha wananchi kuwa wanaweza kupata/kufikia maboresho ya uhakika katika upatikanaji wa huduma kwa juhudi zao wenyewe,mradi unachangia katika kuanzisha utamaduni wa uwakilishi wa wananchi na kuleta manufaa katika nyanja mbalimbali. 
 
Fungua ukurasa wa wazo la mwanzo la mradi (pdf).
  
Utangulizi
 
Upatikanaji wa maji safi na salama katika maeneo ya vijijini Tanzania umekuwa ukishuka katika miaka ya hivi karibuni. Wakati huo huo watanzania walio vijijini wanasema upatikanaji wa maji ni hitaji lao la kipaumbele kwa serikali, na kuipa sekta ya maji vigezo vya chini vya uridhishaji kuliko sekta nyingine za huduma za kijamii, Serikali ya nchi imeshachukua hatua kutatua hili tatizo, kwa kuongeza fungu la fedha kwa ajili ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijni kwa zaidi ya asilimia 40 tangu mwaka 2006. 
 
Lakini, changamoto za usawa na uendelevu zimekuwepo kuzuia fedha hizo katika kufikia malengo yanayotakiwa.Utambuzi wa vya vyanzo vya maji uliofanywa na WaterAid Tanzania umeonyesha kuwa asilimia 54 tu ya vyanzo vya maji vinafanya kazi.na kwa kuchanganya taarifa zinazofanana na utambuzi huo na na taarifa ya bajeti ya serikali za mitaa,TAWASANET iligundua kuwa sehemu kubwa ya fungu jipya la fedha linaelekezwa kwa jamii ambazo tayari zina huduma nzuri ya maji ukilinganisha na sehemu zingine.
 
Wizara ya Maji na umwagiliaji imetambua umuhimu wa dhana yakuweka ramani katika vyanzo vya maji ambayo ilitumika katika tambuzi za WaterAid kama msingi wa mfumo wa ufuatialiji ulioboreshwa kwa sekta ya maji.Matokeo yake mfumo  wa ufuatiliaji wa miundombinu  maji wa taifa sasa unaanzishwa katika misingi ya kuweka ramani kwenye vyanzo vya maji..Hii itajumuisha kufanya tambuzi za awali kitaifa na kuweka mfumo wa taarifa na mtandao kwa upatikanaji rahisi wa taarifa. Vyote mifumo ya taarifa na komputa zinatarajiwa kuwa tayari kakitati ya mwaka 2010.
 
Utambuzi wa vyanzo vya maji unatoa nafasi muhimu kama njia ya  kuhamasisha au kuongeza uwakilishi wa wananchi na na uwajibikaji kwa serikali.Mradi ulioelezwa kwenye kurasa/karatasi hii unalenga kuunganisha uwekaji ramani wa vyanzo vya maji na teknolojia ya simu n ushirikiano wa vyombo vya habari ili kuwezesha au kufanikisha mpango huu.
 
Mradi: Kutia Presha ya Maji
 
Mradi unalenga katika kupandisha au kuongeza uwakilishai wa wananchi na kuongeza uwajibikaji wa seikali za mitaa, hivyo kuleta maboresho yanayoonekana katika usawa na uendelevu wa upatikanaji wa huduma ya maji vijijini.
 
Lengo kuu:
                Kuongezeka kwa upatikanaji wa maji safi na salama Tanzania vijijini 

Malengo
:
  1. Kuongezeka kwa kiwango cha utendaji wa vyanzo vya umma vya maji vilivyoboreshwa maeneo ya vijijini.
  2. Kuwepo zaidi kwa mgawanyo sawa wa uwekezaji wa umma katika usambazaji wa maji vijijiini ndani ya wilaya.
  3. Nguvu ya uwakilishi wa wananchi katika kuleta maboresho yanayoonekana katika upatikanaji maji vijijini unaonekana na unatambuliwa.
 
Sehemu za mradi
 
Mradi umeanzishwa katika msingi mkuu wa kazi wa kuhamasisha juhudi za wananchi;kutoa/kuweka taarifa wazi,mfumo wa urejeshaji taarifa kupitia ujumbe wa wananchi na ushirikiano wa vyombo vya habari kwa uwajibikaji. Hivi vipengele vitapewa nembo ya utambulisho ili kutambulika kirahisi.  
 • Kutoa au kuweka taarifa wazi – Mradi utafanya taarifa zinohusu upatikanaji wa maji vijijini zipatikane na zieleweke kirahisi kwa wananchi kadri inavyowezekana.Hii inajumuisha  taarifa kutoka  utambuzi wa uwekaji ramani wa vyanzo vya maji katika hali halisi ya upatikanaji wa huduma ya maji vijijini na juu ya tarifa wazi na sahihi kuhusu sera za taifa na fedha za sekta ya maji.
   
 • Mfumo wa urejeshaji taarifa kupitia ujumbe - Mbinu rahisi itaanzishwa kwaajili ya wananchi kutumia simu zao kutoa taarifa juu ya upatikanaji maji vijijini.Taarifa zitakazotolewa na wananchi zitapelekwa kwa mamlaka husika za serikali na vyombo vya habari hivo kuviwezesha viweze kitikia au kuwajika kwa haraka.
   
 • Ushirikiano na vyombo vya habari – Mradi utatumia ushirikiano wa vyombo vya habari vya kitaifa na kawaida ktoa afasi kwa majadiliano/midahalo ya umma kuhusu upatikanaji wa maji vijijini na kutia msukumo kwa wawakilishi waliochaguliwa na viongozi wa serikali zakuitikia/kuwajibika ipasavyo. Taarifa inayotumwa ni ya wananchi kupitia mfumo wa kutuma ujumbe.
   
Ratiba ya Utekelezaji
 
Utekelelezaji wa ratiba ya maka mitatu umegawanyika katika awamu kuu mbili-jaribio la mwanzo la kuanzisha na kujaribisha vipengele muhimu vya mradi katika wilaya tatu ambazo taarifa tayari zipo katika mwaka wa kwaza,ikifuatiwa na miaka miwili ya utekelezaji kitaifa. 
 
Wahusika katika Utekelezaji
 
Utekelezaji wa mradi utaongozwa na Daraja,pamoja na  ushirikiano wa vyombo vya habari kiwilaya na kitaifa.Ushirikiano zaidi unaanzishwa ili kukuza/kutanua na kujikita kiundani kwenye mradi kwa matokeo/mafanikio makubwa zaidi.