Kazi Zetu‎ > ‎

Mradi wa Utafiti wa Ushauri wa Sera

Mradi huu umeanzishwa na kazi ya Daraja ya serikali za mitaa kufanya utafiti jinsi ambavyo sera za taifa zinavyotafsiriwa kivitendo/zinavyotekelezwa. Utafiti huu utatumika kutoa ushauri kwa serikali ya taifa juu ya sera zinazoweza kuongeza uwajibikaji wa serikali za mitaa.
 
Kwa mfano ni uwezo gani mamlaka za serikali za mitaa zinao? Je zinapewa nafasi ya kufanya maamuzi kuendana na mahitaji/matakwa ya jamii au maumuzi yao yanabanwa na serikali kuu? Na nini serikali kuu inaweza kufanya rahisi kwa wananchi,na asasi za kiraia kuhoji maamuzi yanayofanywa na serikali za mitaa?
 
Baadhi ya tafiti zimekwishafanyika chini ya mradi huu na zingine zipo njiani au zinaandaliwa, japo mradi unatarajiwa kuanza katikati ya mwaka 2010.