Kazi Zetu

Daraja linapambana na umaskini kwa kufanya serikali za wilaya na mitaa zifanye kazi kwa nguvu zaidi. Tunaamini kwamba bila kuzingatia zaidi maslahi na matakwa ya jamii, fedha zilizotengwa kwa ajili ya kuboresha mashule, vituo vya afya, vituo vya maji na barabara hazitatumika vizuri. Tunashirikiana na serikali pamoja na wananchi ili mapendekezo ya jamii yanasikika na kutekelezwa zaidi. Njia zetu za kazi zinaelezwa zaidi hapa.
 
Mkatati wa 2010-2013
 
Katika mkakati wetu wa 2010-2013, Kazi ya Daraja imegawanyika katika miradi mitatu, kila moja ikiwa inalenga utawala bora kwa njia tofauti. Miradi hii mitatu inaelezwa zaidi hapa (download).
 
Kuongeza Presha ya Maji (Raising the Water Pressure) ni mradi wa kitaifa unaolenga kuboresha utawala katika sekta ya maji vijijini. Mradi huu unaweka njia zilizo rahisi kwa mwananchi wa kawaida kutoa taarifa juu ya matatizo katika vituo vyao vya maji. Hivyo, mradi unasaidia Idara za Maji za Halmashauri za Wilaya kujua matatizo yaliyopo katika maeneo yao na kutatua matatizo haya kwa haraka zaidi. 
 
Twende Pamoja ni mradi wa kuongeza nguvu ya vyombo vya habari wilayani na vijijini. Kwanza, mradi utaanzisha gazeti la jaribio katika mji na wilaya ya Njombe. Gazeti hili litakuwa kama jukwaa la jamii: sehemu kwa jamii zima kuzungumzia matatizo na mahitaji yao, kuchambua kazi za halmashauri ya mji na wilaya, na kuboresha mawasiliano kati ya serikali na wananchi.  
 
Mradi wa Utafiti na Ushauri ni mradi unaoangalia utekelezaji wa sera za kitaifa katika ngazi ya wilaya. Tutafanya utafiti juu ya hali halisi ya sera za taifa zikifika wilayani, na kutumia utafiti huu kutoa ushauri kwa serikali ya taifa juu ya namna kuboresha sera za taifa ili maslahi ya wananchi yazingatiwe zaidi.
 
Kazi za Awali
 
Kabla ya 2009, Daraja haikuwa na wafanyakazi. Kazi zetu zilikuwa zaidi katika mfumo wa utafiti pamoja na miradi ya majaribio.