Bodi ya Wakurugenzi Tanzania

Kajubi Mukajanga (Mwenyekiti wa Bodi) ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (Media Council of Tanzania), iliyoanzishwa kwa ajili ya kuboresha na kulinda uhuru wa vyombo vya habari. Kabla ya hapo alikuwa mchambuzi wa sekta ya utoaji habari.

Francesca Matay (Mtunza Hazina) ni mkurugenzi na mwanzilishi wa Tanzania Women of Impact Foundation (TAWIF), shirika linalopigania haki za wanawake na utawala bora. Ana digrii ya Masters ya Uchumi.

Josephine Lemoyane ana uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika miradi tofauti ya maendeleo hapa Tanzania, zikiwemo miradi ya DFID. Kwa sasa anafanya kazi kama mshauri wa utawala bora katika shirika la SNV.

Moses Kulaba ni mwanaharakati mwenye moyo ya kuziongezea nguvu asasi zisizo za kiserikali kufanya serikali iwajibike. Kwa sasa anafanya kazi katika shirika za Norwegian Church Aid (NCA), NGO Policy Forum, na kama Katibu Mtendaji wa Agenda Participation 2000 (AP2000), shirika linalolenga kuongeza mchango wa jamii katika kuandaa mipango ya serikali. Katika kazi zake za AP2000, Moses ni kiongozi wa Mfumo wa Ufuatiliaji wa Rushwa (Corruption Tracker System).

Salvius Nkwera ni mchumi anayefanya kazi na serikali za mitaa Tanzania. Kwa sasa yupo Dar es Salaam, lakini kabla ya hapo alikuwa katika wilaya ya Makete kama Afisa Mipango ya Wilaya.