Wafanyakazi Tanzania

Ben Taylor ni Mkurugenzi Mtendaji wa Daraja na kiongozi wa Daraja Tanzania. Ben amefanya kazi kwa miaka 9 katika miradi mbalimbali za maendeleo na utawala bora. Hivi karibuni alikuwa WaterAid, akiwa anaongoza kitengo cha utafiti na ushauri. Kazi zake WaterAid ni pamoja na kufanya sekta ya maji izingatie zaidi maslahi na matakwa ya jamii kwa ujumla, hasa walio vijinini. Kabla ya hapo, alifanya kazi katika shirika la Students' Partnership Worldwide (SPW) katika mkoa wa Iringa kwa miaka mitano, akiongozi mradi wa kutoa elimu kwa vijana juu ya afya ya uzazi pamoja na maendeleo ya jamii.

Digrii yake ya kwanza ni kutoka Chuo Kikuu cha Oxford, Uingereza. Pia, ana digrii ya Masters katika Menejimenti ya Maendeleo kutoka Taasisi ya Sera na Menejimenti ya Maendeleo (Institute for Development Policy and Management, IDPM) katika Chuo Kikuu cha Manchester, Uingereza. Maada ya utafiti wake ulikuwa utekelezaji wa sera za Tanzania juu ya uratibu wa miitikio ya UKIMWI vijijini.