Kuhusu Daraja

Daraja ni shirika lililoanzishwa hivi karibuni, linalofanya kazi katika maeneo ya vijijiini Tanzania kwa nia ya kufanya serikali za mitaa na wilaya zizingatie zaidi maslahi ya jamii.
 
Madhumuni yetu ni kuziwezesha jamii na asasi zilizoko vijijini na kuzijengea uwezo wa kufanya kazi kwa ushirikiano wa karibu ili kupunguza umaskini nchini Tanzania. Tunaamini kuleta serikali karibu zaidi na wananchi, na tunalenga kuhakikisha kuwa mfumo wa demokrasia katika ngazi za vijiji na wilaya unaleta mafanikio kwa jamii nzima, hasa kwa wanyonge.
 
Makao makuu ya Daraja yapo katika mji wa Njombe, mkoani Iringa. Hii inasaidia kuhakikisha kuwa kazi zetu zinazingatia hali halisi ya maisha ya vijijini. Njombe na maeneo yaliyo karibu na Njombe ni eneo la kubuni na kuboresha mawazo yetu kabla ya kuyafanyia kazi kitaifa.
 
Tayari tumeweza kupata jina zuri kwa kazi zetu bunifu katika utawala bora wa serikali za wilaya na mitaa. Utafiti wetu umeshachapishwa mara mbili na shirika la HakiElimu kama working papers. Pia tulichangia sura juu ya utaratibu wa bajeti ya serikali za wilaya katika muuongozo wa mchakato wa bajeti  yaTanzania( the Guide to the Budget Process in Tanzania), kilichoandaliwa na Policy Forum.
 
Tunaona umuhimu wa kufuata/kushikilia miiko/madhehebu yetu katika kazi zetu zote. Kwa mfano, kama vile lengo letu ni kufanya serikali izingatie zaidi maslahi ya jamii, ni lazima na sisi pia tusisahau kusikiliza na kujielezea kwa uwazi kwa jamii. Hivyo, tovuti hii inatumika kama ubao wa matangazo juu ya kazi zetu zote, hasa ripoti zetu zote za mwaka, zikiwemo ripoti za matumizi wa fedha, pamoja na katiba yetu, nk. Angalia kurasa za uwazi na uwajibikaji.
 
Daraja Development Limited limesajiliwa Tanzania mwaka 2009 kama kampuni lisilo la kutegeneza faida kipesa (Namba 71414). Linaongozwa na Bodi ya Wakurugenzi wenye uzeofu mwingi katika kazi za maendeleo pamoja na utawala bora. 
 
Daraja Trust ni shirika-dada la Daraja Development Limited, lililosajiliwa Uingereza kama shirika la hisani (Namba 1116346). Daraja Trust lina Bodi ya Wadhamini wenye uzoefu wa kazi za maendeleo ya jamii, hasa nchini Tanzania.
 
Mashiriki haya mawili yanashirikiana lakini kila moja linajitegemea.
 
Tumia vichwa vya habari vifuatavyo ili kufahamu zaidi kuhusu Daraja:
  • Sisi ni nani? Soma kuhusu wafanyakazi wetu, wakurugenzi na wadhamini
  • Ripoti na mahesabu Vitu hivi viwili vipo kwa ajili ya kufuata/kushika miiko/ madhehebu yetu ya uwazi na uwajibikaji
  • Daraja katika taarifa za habari. Bonyeza hapa ili uone ni jinsi gani Daraja ilivyotangazwa katika vyombo vya habari vya Tanzania na Uingereza.
  • Nafasi za Kazi. Soma kuhusu nafasi za kazi katika shirika la Daraja.