Daraja ni shirika lisilo la kiserikali lenye madhumuni ya kuleta mabadiliko katika jamii za Watanzania wanaoishi vijijini kwa kujenga mahusiano ya karibu zaidi kati ya wananchi na serikali. Jina letu Daraja, maana yake ni kuunganisha pande hizi mbili yaani wananchi na serikali.
 
Serikali za mitaa na za wilaya zinawajibu wa kusikiliza mawazo ya wanajamii na kusimamia huduma za jamii zinazoendana na mahitaji na matakwa ya wananchi. Daraja inataka kuhakikisha kuwa serikali hizo zinatimiza huo wajibu ipasavyo.
 
Tumia vichwa vya habari hapo kulia ili kujua zaidi kuhusu Daraja - sisi ni nani, tunafanya kazi gani, misingi ya kuanzisha Daraja, nk.
 
Daraja Development Limited ni shirika lisilo la kiserikali, lililosajiliwa Tanzania kama kampuni lisilo lisilotengeneza faida ya kifedha (Namba 71414). Pia, Daraja Trust (shirika dada la Daraja Development Limited) limesajiliwa Uingereza kama shirika la Kihisani (Namba 1116346).